
Je, Unajua? Mtindo Wako wa Maisha Leo Unaweza Kukusababishia Matatizo ya Tezi Dume Kesho.
Ukiachana na sababu za kurithi, kuna baadhi ya tabia unazoishi nazo sasa ambazo zinaweza kukupeleka moja kwa moja kwenye matatizo ya tezi dume kadri umri unavyosonga.
Lakini je, unaelewa maana halisi ya kuwa na tatizo la tezi dume? Au ukiambiwa una saratani ya tezi dume, unajua inamaanisha nini kwa afya yako na maisha yako kwa ujumla?
IPO HIVI....
Tezi dume sio ugonjwa bali ni kiungo katika mwili wa mwanaume, kama inavyo fahamika (Tezi dume).
Tezi dume sio bushaa, Hili unatakiwa kulifahamu kwani watu wengi wanashindwa kutofautisha kati ya tezi dume na busa.
Kazi kubwa ya Tezi dume kwa mwanaume ni kutengeneza maji maji yaani shahawa, Zinazo saidia mbegu zakiume kuogelea katika safari ya kurutubisha yai kwa mwanamke Na mbegu kubaki na uhai.